Tafuta maeneo yenye vipengele vya ufikiaji
Tunaamini kuwa mtu yeyote anaweza kujisikia nyumbani mahali popote—na tungependa kufanya iwe rahisi kwa watu wenye ulemavu na mahitaji mengine ya ufikiaji waweze kusafiri.
Sasa unaweza kutafuta mlango mpana, eneo lisilo na ngazi, au vipengele vingine vya ufikiaji ili kukusaidia kupata eneo linalokidhi mahitaji yako.
Vipengele vya ufikiaji
Hivi ndivyo vipengele unavyoweza kuchuja kulingana na:
- Ufikiaji usio na ngazi
- Mlango wa mgeni wenye upana wa zaidi ya inchi 32
- Maegesho ya walemavu
- Ufikiaji wa chumba cha kulala bila ngazi
- Mlango wa chumba cha kulala wenye upana wa zaidi ya inchi 32
- Mlango wa kuingia bafuni usio na ngazi
- Mlango wa bafu wenye upana wa zaidi ya inchi 32
- Kiti cha kuogea
- Bafu lisilo na ngazi
- Chuma cha kujishikilia cha chooni
- Chuma cha kujishikilia cha bafuni
- Kifaa cha kumwinua mtu kinachoning'inia darini au kinachosogezwa
Chuja kulingana na vipengele vya ufikiaji:
- Weka mahali uendako, tarehe za kusafiri na idadi ya wageni
- Mara matokeo yako ya utafutaji yanapoonekana, bofya Vichujio
- Nenda kwenye Vipengele vya ufikiaji kisha ubofye Onyesha zaidi
- Chagua vipengele unavyotaka kisha ubofye Onyesha sehemu
- Weka mahali uendako, tarehe za kusafiri na idadi ya wageni
- Mara matokeo yako ya utafutaji yanapoonekana, gusa Vichujio
- Nenda kwenye Vipengele vya ufikiaji kisha uguse Onyesha vipengele vyote vya ufikiaji
- Chagua vipengele unavyotaka kisha uguse Onyesha sehemu
- Weka mahali uendako, tarehe za kusafiri na idadi ya wageni
- Mara matokeo yako ya utafutaji yanapoonekana, gusa Vichujio
- Nenda kwenye Vipengele vya ufikiaji kisha uguse Onyesha vipengele vyote vya ufikiaji
- Chagua vipengele unavyotaka kisha uguse Onyesha sehemu
- Weka mahali uendako, tarehe za kusafiri na idadi ya wageni
- Mara matokeo yako ya utafutaji yanapoonekana, gusa Vichujio
- Nenda kwenye Vipengele vya ufikiaji kisha uguse Onyesha zaidi
- Chagua vipengele unavyotaka kisha uguse Onyesha sehemu
Mahali pa kupata taarifa ya ufikiaji kwenye tangazo
Kwa kuwa sasa umepata tangazo linalokidhi mahitaji yako, hapa ndipo unapoweza kupata maelezo zaidi kuhusu vipengele vya ufikiaji vya eneo hilo.
- Maelezo ya tangazo: Wenyeji mara nyingi huweka taarifa ya ufikiaji katika maelezo ya tangazo
- Sehemu ya ufikiaji: Wenyeji wanatoa picha za vipengele vya ufikiaji kwenye eneo lao
- Wasiliana na Mwenyeji: Iwapo ungetaka kupata maelezo zaidi kuhusu vipengele vya ufikiaji kwenye eneo, tumia kitufe cha Wasiliana na Mwenyeji
Sera ya Kutobagua
Kama sehemu ya kujizatiti kwetu kuhusu ujumuishaji na heshima kwa kila mtu katika jumuiya yetu, Sera yetu ya Kutobaguahaiwaruhusu Wenyeji kumkataa mgeni kwa sababu tu ana ulemavu. Tunajitahidi kuifanya jumuiya ya Airbnb iwe rafiki zaidi kwa walemavu kwa kuwapa Wenyeji na wageni fursa za kushiriki taarifa za ufikiaji.
Makala yanayohusiana
Kupata sehemu ya kukaa inayokufaa
Unataka msaada wa kupata sehemu nzuri ya kukaa? Haya ni maeneo maarufu ambayo wageni huulizia wanapotafuta safari yao inayofuata.- Mgeni
Thibitisha nambari yako ya simu
Mara baada ya kuweka nambari yako ya simu kwenye akaunti yako, basi wageni, wenyeji na Airbnb wanaweza kuwasiliana nawe kuhusu nafasi uliyow… Kuunda akaunti yako
Umeingia, lakini unahitaji kuhariri akaunti yako. Unaenda wapi? Hivi ndivyo unavyoweza kusasisha wasifu wako, kusimamia mipangilio ya arifa …